Diamond aeleza sababu ya kuchukua 60% ya mapato ya wasanii WCB

0
27

Kufuatia kuondoka kwa Rayvanny wiki mbili zilizopita, ambaye alilazimika kulipa TZS bilioni 1 ili kununua sehemu iliyobaki ya mkataba wake wa miaka 10, kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inavyowachukulia wasanii wake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, mmiliki wa lebo hiyo, Diamond Platnumz amesema haoni tatizo kuhusu mkataba huo ambao wengi wanadai kuwa ni mkataba wa ‘kinyonyaji’ ambao unaifanya WCB kuchukua asilimia 60 ya mapato yote yanayotokana na kila msanii aliyesajiliwa chini ya lebo hiyo.

Diamond Platnumz amesisitiza kwamba alipowachukua wasanii hao hawakuwa na chochote mikononi mwao, na ilikuwa sahihi kurejesha mamilioni aliyowekeza kwao.

“Tuweke kitu kimoja sawa, muziki ni biashara. Wanaolalamika tunawanyonya wasanii wanaonekana kusahau wasanii hawa walikuwa kwenye lebo nyingine tofauti lakini hawakuwa maarufu. Tuliwachukua, na tukawatengeneza hadi wakafikia hatua ya kuuzika na kuzalisha pesa nzuri tofauti na ilivyokuwa hapo awali. WCB tuliwafanya kuwa matajiri na maarufu na unawasikia wanathibitisha,” Diamond Platnumz.

Ameongeza “Hakuna wasanii matajiri Tanzania baada yangu, zaidi ya wale wa WCB. Nilifanya haya kwa kuwekeza mamilioni ya pesa zangu kwao, lakini sasa msanii anapoanzishwa, anataka kukimbia na biashara nzima. Siwezi kuruhusu hilo, ilibidi nirudishiwe pesa zangu na faida pia.

Mwimbaji huyo amesema, aliwekeza zaidi ya TZS milioni 600 kwa msanii Rayvanny pamoja na Harmonize ili kuwatengeneza kimuziki.

Send this to a friend