Diamond: Vanessa aliposaini Universal Music Group nilijua ataumia

0
31

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kwa jina la sanaa, Diamond Platnumz amezungumzia uzoefu alioupata kwa kufanya kazi kwa miaka minne na Universal Music Group na kwamba amepata mafanikio pamoja na kujifunza mengi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, nyota hiyo amesema kwamba aliposikia mwanamuziki mwenzake Vanessa Mdee ameingia mkataba na kampuni hiyo amesema alitamani amwambie anachoenda kukutana nacho.

“Nisiwe mnafiki napomuona msanii yeyote anaposaini [na Universal Music Group] kwa mara ya kwanza, namsikitikia… Dada yangu Vanessa [Mdee] aliposaini niliuambia uongozi, duh! Natamani ajue anachoenda kukutana nacho,” amesema Diamond.

Msanii huyo anayefanya vizuri kwa nyimbo mbalimbali zikiwamo Jeje na Baba Lao, amesema kuwa amejifunza mengi wa kusaini na lebo hiyo na licha ya kuwa baadhi ya mambo hayakwenda kama alivyokuwa ametarajia, anaamini akisaini mkataba mwingine au msanii wa WCB akitaka kusaini mkataba, basi utakuwa bora zaidi.

Katika hatua nyingine Diamond ametangaza kuwa meneja wake, Sallam SK atakuwa Balozi wa Universal Music Group kwa Afrika Mashariki, na anaamini kwa vile anafahamu muziki wa kanda hii, basi ataboresha zaidi.

Send this to a friend