Diamond: Wakati mwingine tutashinda BET

0
47

Mwanamuziki Diamond Platnumz amewashukuru Watanzania kwa upendo na umoja waliomuonesha katika kipindi chote cha kuwania tuzo ya BET nchini Marekani.

Diamond ametoa shukrani hizo saa chache baada ya tuzo hizo kutolewa na Burna Boy kutoka Nigeria kuibuka mshindi katika kipengele alichokuwepo.

“Kupitia tuzo hii nimeona ni kiasi gani Watanzania tuna umoja, upendo na kuthamini vya kwetu. Nawashkuru sana kila mmoja wenu kwa upendo mkubwa mlionionesha,” ameeleza mwanamuziki huyo.

Akizungumzia kukosa tuzo hiyo, amesema “Naamini wakati mwingine tutaibeba.”

Aidha, amewaomba Watanzania kumuunga mkono msanii yeyote atakayekuwa analiwakilisha Taifa katika jambo lolote kwani Tanzania ni moja.

Diamond alikuwa akiwania tuzo ya Msanii Bora wa Kimataifa (Best International Act) ambapo alikuwa akichuana na Burna Boy, Wizkid, Emicida, Headie, Aya Nakamura, Youssoupha na Young T & Bugsey.

Send this to a friend