Dirisha la Pili la Nuru Yangu Scholarship and Mentorship Program chini ya NMB Foundation limefunguliwa rasmi kwa mwaka wa masomo 2023/24 πŸ“šπŸ‘¨πŸΎβ€πŸ«πŸ§‘πŸΎβ€πŸ«

0
45

Ufadhili huu wa masomo ya shahada hutolewa kwa wanafunzi wenye ufaulu mzuri kwenye mitihani yao ya kidato cha sita lakini wanatoka kwenye mazingira magumu na hawana uwezo wa kujisomesha.

Zaidi ya ufadhili wa masomo, vijana hawa watapata mafunzo ya vitendo katika benki yetu na makampuni mengine washirika.

Kwa mwaka huu, tumetenga zaidi ya Tsh Bilioni 1 kwaajili ya wanafunzi 130 (65 wa mwaka jana na 65 wa mwaka huu) kugharamia :
βœ… Ada
βœ… Fedha za Kujikimu
βœ… Fedha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo
βœ… Gharama zote zinazolipwa kwa chuo
βœ… Vifaa vya shule
βœ… Kompyuta mpakato (laptops)

Uzinduzi huu umefanywa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB Foundation – Bi. Ruth Zaipuna pamoja na Meneja Mkuu wa NMB Foundation – Nelson Karumuna.

Kwa wale wenye vigezo, wanaweza kujisajili kupitia foundation.nmbbank.co.tz kabla ya Oktoba 8, 2023 na safari ya kutimiza ndoto ianze.

#NMBKaribuYako

Send this to a friend