Diwani aliyepotea kutengenezea filamu tukio lake (Lost and Found Tour)

0
62

Diwani wa Kawe aliyepotea na kupatikana Mei 23 mwaka huu, Mutta Rwakatare amesema anatarajia kuitengenezea filamu tukio lake la kupotea huku akilifananisha tukio hilo na filamu ya ‘Lost and Found Tour.’

Ameyasema hayo wakati alipohojiwa na vyombo vya habari baada ya kuhudhuria kikao cha kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla, Kinondoni Jijini Dar es salaam.

“Niseme kilichotokea kimetokea kwa sababu ambayo imesaidia mimi kujifunza kitu na kuifunza jamii pia, naiita Tour ya Lost and Found na nina mpango wa kulitengenezea movie tukio hili” amesema Mutta.

Aidha, kwa upande wake Makalla amesema mwanamke anayedaiwa ‘alimteka’ Mutta anayefahamika kwa jina la Ashura, anamfahamu na aliwasiliana naye wiki moja kabla ya tukio hilo kutokea.

“Ashura mimi namfahamu alinipigia simu wiki moja kabla ya tukio kunielezea masuala yake binafsi ya kurudi nchini akitokea Ujerumani. Hata hivyo baada ya tukio la Mutta kutokea na kupiga simu kuona namba inayotokea ni yake, ilibidi nimhoji kulikoni kufanya hivyo na alinielezea yote na kubaini kuwa hakuwa mtekaji kama watu wanavyosema,” ameeleza RC Makalla

Mutta ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wapiga kura wake, wananchi na viongozi kwa ujumla na kuahidi kuwa hatopotea tena.

Send this to a friend