Diwani aliyepotea kwa miezi mitatu akutwa kwa mwanamke Tabata

1
60

Jeshi la Polisi limesema Diwani wa Kata ya Kawe, Mutta Mwakatare (43) mkazi wa Mikocheni Kinondoni aliyetoweka tangu Februari mwaka huu amepatikana.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Muliro J. Muliro amesema walifanya ufuatilliaji wa taarifa hizo na kufanikiwa kumpata Mei 23 mwaka huu akiwa kwenye nyumba ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Ashura Matitu (43) mkazi wa Tabata Darajani.

Mwanamke huyo alidai kuwa diwani huyo ni rafiki yake wa siku nyingi kwa zaidi ya miaka 10 na alifika nyumbani kwake tarehe 19/05/2022 akiwa katika hali ya ulevi uliopitiliza.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema kutokana na mazingira ya ulevi ambayo diwani amekutwa nayo, pia ndugu zake walitoa kumbukumbu za nyuma, mwenendo na tabia za diwani huyo hivyo Jeshi la Polisi limemkabidhi kwa ndugu zake kwa matibabu na tiba zaidi za kisaikolojia.

Send this to a friend