Dkt. Kikwete: Niliuona uwezo wa Rais Samia kiuongozi tangu 2001

0
58

Rais Mstaafu Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefichua sababu inayomfanya ajivunie Rais Samia Suluhu Hassan kama kiongozi wa Taifa la Tanzania kuwa ni uwezo alionao kwenye masuala ya uongozi.

Akijibu swali kuhusu utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita katika mkutano uliohusu hali ya Demokrasia barani Afrika uliofanyika jijini Arusha, Dkt. Kikwete amesema aliuona uwezo wa Rais Samia katika uongozi tangu mwaka 2001 na jinsi anavyoweza kukabiliana na changamoto.

“Ndiyo, ninajivunia sana Samia kama Rais wetu. Niliuona uwezo wake wa uongozi tangu mwaka 2001,” amesema Kikwete.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Kikwete alimteua Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais.

Rais Samia: Ukosefu wa huduma za msingi unaibua migogoro

Hata hivyo, katika kipindi cha mwisho cha utawala wake mwaka 2015, Dkt. Kikwete alikiri kwamba alimshawishi marehemu John Pombe Magufuli, mgombea urais wa CCM, kumchagua Mama Samia kama mgombea mwenza.

Send this to a friend