Dkt. Luhende ateuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali

0
76

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali, kabla ya uteuzi huo Dkt. Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Dkt. Boniphace Luhende anachukua nafasi ya Gabriel Paschal Malata ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Aidha, Rais Samia amemteua Bi. Sara Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mwaipopo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Send this to a friend