Dkt. Mollel: Serikali inalifanyia kazi suala la sheria kuruhusu utoaji mimba

0
19

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa, matatizo yatokanayo na utoaji mimba ni moja ya sababu inayochangia vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 10.

Kauli hiyo imebainishwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel jijini Dodoma wakati akijibu maswali bungeni kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Hata hivyo, amesema madhara yanayotokana na utoaji wa mimba usio salama ni pamoja na maambukizo makali ya mfumo wa uzazi (Septic Abortion) ambao unaweza kupelekea mgonjwa kutolewa mfuko wa uzazi na wakati mwingine kupoteza maisha.

Sita wafariki na watano wapatwa na upofu kwa kunywa pombe iliyokwisha muda wake

Aidha, akijibu kuhusu sheria kuruhusu utoaji mimba ulio salama kutokana na sababu mbalimbali muhimu, amesema Serikali inaendelea kuchakata suala hilo ili kuepuka kufanya makosa.

“Inahitaji mchakato mkubwa kwa sababu inagusa wizara mbalimbali lakini inagusa imani mbalimbali za watu na mambo mengine, tupeni muda tuendelee kuchakata ili tusije kujaribu kuzuia tatizo kwa namna nyingine tukazalisha tatizo lingine,” ameeleza.

Send this to a friend