Dkt. Mpango aiagiza TLS kuwachukulia hatua mawakili wanaopokea rushwa

0
42

Makamu wa Rais, Philip Mpango ametoa wito kwa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Kamati ya Mawakili kuchukua hatua kali za kinidhamu na kisheria dhidi ya baadhi ya mawakili wanaoharibu heshima ya taaluma ya sheria kwa kukosa uadilifu na maadili mema.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TLS unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Dkt. Mpango amesema kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya mawakili kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kuwasaliti wateja kwa kupokea rushwa kutoka upande wa pili na kuharibu kesi.

Waziri Mkuu: Tunazungumza na Denmark wasifunge ubalozi wao nchini

Aidha, Dkt. Mpango ametoa rai kwa TLS kuhakikisha inashirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kutoa elimu kwa umma kuhusu suala la mihuri ya kielektroniki ili kuondokana na suala la vishoka na mawakili wanaotumia mihuri isiyo halali kufanya kazi za uwakili.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wake wanatendewa haki kwa mujibu wa sheria na kuishi kwa amani na utulivu katika nchi yao.

Send this to a friend