Dkt. Mpango akemea baadhi ya mawakala RUWASA kutumia mitambo ya serikali kufanyia biashara

0
38

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amekemea baadhi ya Mawakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kutumia Mitambo ya uchimbaji visima iliyonunuliwa na serikali kwa matumizi yao binafsi.

Amesema hayo wakati akikagua magari na mitambo ya uchimbaji visima na mabwawa yaliokabidhiwa kwa RUWASA wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2021/2022 iliyofanyika jijini Dar es Salaam Machi 20, 2023.

Katika hotuba yake, Dkt. Mpango  ameiagiza RUWASA kutambua kuwa  wanapaswa kutoa huduma zaidi kwa wananchi zilizokusudiwa ikiwemo kutoa huduma kwa gharama nafuu.

Aidha, Makamu wa Rais ameagiza kufanyika tathmini ya bei zinazotumika na RUWASA kuchimba visima binafsi vya wananchi ili kuhakikisha haziwi juu zaidi ya bei za kampuni binafsi.

Send this to a friend