Dkt. Mpango azindua maabara ya afya ya jamii Kibong’oto

0
15

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo tarehe 16 Julai 2022 amefungua maabara ya afya ya jamii ya Kibong’oto wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, iliyogharimu shilingi bilioni 12.5.

Katika hotuba yake mara baada ya ufunguzi wa maabara hiyo, amesema ujenzi wa maabara ya afya ya jamii katika hospitali hiyo utaboresha huduma za tiba na udhibiti wa magonjwa nchini pamoja na kupunguza gharama kwa Serikali kupeleka sampuli nje ya nchini.

Dkt. Mpango ameitaka Wizara ya Afya kuendelea kuimarisha mfumo wa ufuataliaji wa mwenendo wa magonjwa ya kuambukiza hasa magonjwa hatarishi ili kupunguza athari zinazoweza kutokea kwa wananchi kutokana na magonjwa hayo.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini magonjwa na kupata tiba mapema. Pia amewasihi madaktari na wahudumu wa afya kote nchini kuendelea kujitoa, kuwa na upendo pamoja na maadili wanapotekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Wizara itaendelea kuboresha huduma za maabara kwa kununua vifaa mbalimbali vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa.

Akizungumzia uwepo wa ugonjwa mkoani Lindi, Waziri Ummy amesema Tanzania ina uwezo wa kuchunguza magonjwa ambukizi na hatarishi kutokana uwepo wa vifaa na wataalamu, hivyo majibu kamili ya ugonjwa ulioibuka yatapatikana.

Amesema tayari wataalamu wa Tanzania wameungana na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kuchunguza ugonjwa huo.

Send this to a friend