Dkt. Mpango kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Marekani

0
64

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewasili Jijini New York nchini Marekani ambapo anatarajia kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA).

Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani Septemba 22, 2022.

Aidha, Dkt. Mpango ataongoza Ujumbe wa Tanzania katika mikutano mbalimbali inayohusu uchumi, elimu, afya, demokrasia na malengo ya maendeleo endelevu ambayo Tanzania imealikwa na nchi washirika, taasisi za kimataifa na asasi binafsi.

Send this to a friend