Dkt. Mpango kumwakilisha Rais kwenye mkutano Uswisi

0
41

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango leo Mei 20, 2022 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Davos nchini Uswisi atakapomwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum).

Mkutano huo utakaofanyika jijini Davos  unaotarajiwa kuanza Mei 22 hadi Mei 26, 2022.

Makamu wa Rais atahudhuria mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya biashara na uwekezaji, ulinzi na usalama, usalama wa chakula, mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na wakuu wa nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara.

Send this to a friend