Dkt. Mpango: Mapenzi ya jinsia moja, hata wanyama hawafanyi

0
60

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwalea watoto kwa kuzingatia maadili ya Kitanzania pamoja na kuongeza umakini katika maudhui yanayooneshwa katika televisheni.

Amesema hayo wakati akizungumza na waumini wa Kijiji cha Kasumo mkoani Kigoma akieleza kuwa ni wazi kwa sasa kumekuwepo na changamoto ya mmomonyoko wa maadili ikiwemo ndoa za jinsia moja ambapo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla inapaswa kukemea vikali ili kuondokana na taifa lisilofaa kwa vizazi vya sasa na baadaye.

BAKWATA: Kifungu kinachoruhusu mtoto wa miaka 14 kuolewa kisiondolewe

“Hili ni gumu kweli, maadili ya nchi yetu yameporomoka sana, yaani na mengine hata kuyasema ni ngumu. Ndoa za wanaume wawili? Ndoa za wanawake wawili? Mliziona wapi? Hata wanyama hawafanyi hivi,” ametahadharisha.

Ametumia jukwaa hilo kuwahimiza wananchi wa Kasumo kutoa ushirikiano wakati huu ambapo serikali inafanya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika mkoa huo ambayo ni nyenzo muhimu kwa biashara na urahisi wa kufikia huduma za jamii kama vile hospitali na shule na kujitolea kwa hali na mali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kijijini hapo ikiwemo ya huduma za afya.