Dkt. Mpango: Serikali inatarajia kupokea ndege mpya mbili

0
41

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema hivi karibuni Serikali inatarajia kupokea ndege mpya mbili aina ya Boeing 737 9 max na Boeing 787 – 8 Dreamliner, ili kuongeza ufanisi kwenye usafiri wa anga nchini.

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua Jukwaa la Kodi na Uwekezaji la mwaka 2024 kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, amesema Tanzania imeendelea kuwa kitovu cha uwekezaji na nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi Kusini mwa Jangwa la Sahara, licha ya misukosuko ya kiuchumi na kijamii inayoendelea duniani kote.

Amesema kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) miradi 526 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.7 [TZS trilioni 14.5] ilisajiliwa nchini kwa mwaka 2023, ikilinganishwa na miradi 256 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.7 [TZS trilioni 9.4] iliyosajiliwa mwaka 2021.

Send this to a friend