Dkt. Mpango: Wapangaji lipeni kodi kwa wakati kuepuka usumbufu

0
21

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa rai kwa wapangaji wanaotumia nyumba za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuzingatia masharti ya mkataba wa upangishaji kwa kulipa kodi kwa wakati ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia mpya ya uwekaji vitasa janja (Smart locks) ambavyo hujifunga pindi mpangaji anapofanya ulimbikizaji wa kodi.

Amesema hayo leo Agosti 04, 2023 mara baada ya kufungua Jengo la Makazi la Kibiashara la TBA lililopo katika eneo la Sekei Jijini Arusha, lililogharimu shilingi bilioni 6.86.

Aidha, amewataka TBA kuhakikisha nyumba zinazojengwa zinakidhi mahitaji ya soko kwa miaka mingi ijayo ikiwemo ubora wa nyumba na sehemu za kupata mahitaji, pia kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yote yanayotekelezwa na kuweka miundombinu sahihi ya ukusanyaji takangumu.

Machinga, bodaboda wamwagia sifa uongozi wa Rais Samia

Vilevile Makamu wa Rais ametoa wito kwa sekta binafsi kushirikiana na TBA katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba nchi nzima, na kuwasihi TBA kuendelea na mpango wa kuyaendeleza maeneo yote yaliyorejeshwa serikalini kwa kujenga majengo ya ghorofa.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutasaidia upatikanaji wa makazi ya uhakika kwa wakazi wa jiji la Arusha, na kwamba mradi huo umesaidia wataalamu wazawa wa fani za ujenzi kujengewa uwezo wa taaluma kwa vitendo.

Send this to a friend