Dkt. Mwigulu: Hakuna haja ya kuhofia tozo ya TZS 100 kwenye mafuta

0
41

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchema amewatoa hofu wananchi kuhusu tozo ya shilingi 100 kwenye kila lita 1 ya mafuta ya dizeli na petroli kwakuwa Serikali inafanya ufuatiliaji wa ndani kwenye soko la dunia kuhusu nishati hiyo ya mafuta.

Akizungumza leo Juni 26, 2023 wakati akihitimisha hoja ya mjadala wa hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali, amesema ikitokea mafuta yameshuka kwenye soko la dunia si mbaya Serikali ikikusanya fedha hizo na kuzielekeza kwenye miradi ya kimkakati.

“Kuna wakati mafuta yamepanda hata sio kwa ajili ya shilingi 100 na Rais akatoa unafuu, sasa kama soko la dunia mafuta yanashuka ile difference [tofauti] Serikali ikikusanya ikatekeleza kwenye miradi kuna shida gani?”

Angalieni kwa nchi nyingine za SADAC na EAC mwone jinsi tofauti ya Rais Samia na maeneo mengine ambavyo walifanya, kwa hapa aliweza kuweka ruzuku bilioni 100 kila mwezi na hapo si kwamba Serikali ilikuwa imepandisha yalipanda kwenye soko la dunia kule,” amesema.

Rais Samia: Serikali yangu si ya maneno ni ya vitendo

Aidha, Dk Mwigulu Nchemba amewatoa hofu Watanzania kuhusu utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati vya binafsi akieleza kuwa hata vya juu walianza na vile vya Serikali kisha vikafuata vyuo binafsi.

“Ni kweli kwamba, tumeanza na waliopangwa vyuo vya kati vya Serikali, waheshimiwa wabunge mtambue kuwa hata kwa vyuo vya juu tulianza na vile vya Serikali ndipo tukaja kwenye taasisi kwa bajeti ya mwakani tutaingia huko,” amesema Dk Mwigulu.

Hata hivyo, baada ya mjadala huo uliofanywa na Dkt. Mwigulu, bunge limeweza kupitisha bajeti hiyo kwa kura 354 sawa na asilimia 95 ya wapiga kura waliokuwepo bungeni kwa kura zote za ndio.

Send this to a friend