Dkt. Mwinyi amhakikishia Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza uchaguzi wa amani na utulivu

0
5

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemshukuru Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Muanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Tony Blair Institute for Global Change (TBI), Sir Tony Blair kwa ushirikiano wake katika sekta mbalimbali ikiwemo kuimarisha bandari, utalii , na kuwajengea uwezo Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Serikalini (PDB).

Dkt. Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Waziri Mkuu Mstaafu huyo, alipomtembelea kwenye makaazi yake The South Pavillion, Cotton Underwood Aylesbury, Uingereza Aprili 06, 2025.

Aidha, Dkt. Mwinyi amemhakikishia kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu katika kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Naye, Waziri Mkuu Mstaafu, Tony Blair amemuahidi Dkt.Mwinyi kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika uchumi wa kidigitali,  utalii, uwekezaji  kupitia Taasisi yake ya TBI.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dkt.Saada Mkuya, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki, Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.