Dkt. Mwinyi aondoa kodi ya sukari Zanzibar

0
37

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye sukari kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuwasaidia wananchi na kuepusha kupanda bei ya bidhaa hiyo.

Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Jumbi na soko la samaki Malindi mkoa wa Mjini Magharibi leo katika ziara maalumu ya kutembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.

Aidha, Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kuacha kupandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi badala yake kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Mwinyi ameisisitiza Taasisi ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki la Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.aon

Send this to a friend