Dkt. Mwinyi asisitiza kutunza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani

0
30

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameisisitiza jamii kuendelea kuitunza amani iliyopo wakati nchi ikielekea katika mwaka wa Uchaguzi Mkuu mwakani.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wa Masjid Shaafy uliopo Mombasa Mbuyu Mnene ,Wilaya ya Magharibi B.

Ameeleza kuwa ni wajibu wa viongozi wa Dini na wanasiasa kuwahubiria amani waumini na wafuasi wao ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu na Serikali iendelee na mipango ya maendeleo.

Aidha, Dkt. Mwinyi amesema kwa miaka minne, nchi imekuwa na utulivu mkubwa, hali inayohitaji kuendelezwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mbali na hayo, Dkt. Mwinyi amefika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lumumba kuwafariji na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo akiwemo Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Haji Machano .