Dkt. Mwinyi: Tamasha la Kizimkazi ni fursa ya utalii na uwekezaji

0
29

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema Tamasha la Kizimkazi ni fursa muhimu kwa Mkoa wa Kusini kuongeza vivutio vya utalii na kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika mkoa huo.

Ameyasema hayo leo katika Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha Dkt. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kumaliza changamoto zinazoukabili Mkoa wa Kusini ikiwa ni pamoja na uhaba wa wafanyakazi sekta ya afya kabla ya kufikia mwaka 2025.

Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa, mbali na kuimarisha utalii wa ndani, tamasha hilo linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi pamoja na kuimarika kwa mila, desturi, na maadili ya Kizanzibari.

Tamasha hilo litaendelea kwa matukio mbalimbali hadi Agosti 25, 2024 ambapo litafungwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Send this to a friend