Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema katika mijadala inayoendelea ya katiba wanaozungumza ni wanasiasa na vyama vya siasa, na si wananchi.
Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari ambapo amesema Serikali inajipanga kuichambua katiba na kutoa elimu kwa wananchi hasa wa ngazi ya chini.
Mambo makubwa matatu ambayo IGP Wambura ataanza nayo
“Kuna wengine hawajawahi kuishika katiba, achilia mbali kuisoma, kwa hiyo anaamini kile ambacho anaambiwa, ni vizuri sasa elimu iwepo, na kwenye hili tunakwenda kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali,” ameeleza.
Aidha, Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa katiba ya nchi ina mapungufu na siyo kwamba haifai, na kwamba Serikali haimzuii mtu yeyote kusema kuwa katiba ina mapungufu.