Dkt. Samia awataka Watanzania kudumisha amani uchaguzi mkuu

0
104

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu amewahakikishia Watanzania kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kulinda amani wakati wote wa uchaguzi.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni Kijiji cha  Kajengwa, Makunduchi Unguja Visiwani Zanzibar, amesema amelazimika kuyasema hayo mara baada ya wazee wa Pemba kumuomba kusimamia amani na utulivu katika uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

“Tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu, ninaowaomba sana twende tudumishe amani na utulivu. Uchaguzi si vita, uchaguzi ni tendo la kidemokrasia ni watu kwenda kwenye utaratibu uliowekwa, kuweka kura zetu, rudi nyumbani katulie ili nchi ibaki salama.

Ameongeza kuwa “Si muda wote kushika silaha kunaleta suluhu ya maana. Niwaombe sana ndugu zangu, amani na utulivu wa nchi yetu ni jambo muhimu kuliko jambo lolote. Hutaki kishindo kapige kura rudi nyumbani tulia.”

Aidha, amesisitiza kuwa ikiwa Watanzania watampa ridhaa ya kuongoza serikali, atahakikisha analinda kwa bidii tunu za Taifa ambazo ni amani, umoja na mshikamano kama sehemu ya kuenzi jitihada zilizofanywa na waasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Amani Abeid Karume.

Send this to a friend