Dkt. Tulia ataja jambo kubwa atakaloanza nalo IPU

0
42

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema moja ya mambo atakayoanza nayo katika nafasi yake ya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ni kuhakikisha anatumia nafasi hiyo kuzishauri na kuzisimamia serikali za nchi mbalimbali duniani kujiepusha na vita.

Ameyasema hayo mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa 31 katika kikao cha Baraza la Uongozi wa IPU kilichofanyika mjini Luanda nchini Angola Oktoba 27, 2023 na kuwa mwanamke wa kwanza Afrika kushika wadhifa huo.

Deni la Kenya kwa Benki ya Dunia lapanda na kufikia TZS trilioni 25

“Nitahakikisha kwamba tunatumia nafasi sisi kama Jumuiya ya Mabunge Duniani kuhakikisha kwamba na sehemu nyingine ambako hakuna amani tunapeleka amani kwa maana ya kuzishauri serikali zetu kujiepusha na mambo ya vita lakini kuzisimamia serikali zetu ili nchi zisiendelee kuingia katika vita,” amesema.

Aidha, Dkt. Tulia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumruhusu kugombea nafasi hiyo ambayo imeiletea heshima kubwa taifa.

Send this to a friend