Dkt. Tulia ayaonya Nipashe na The Guardian upotoshaji suala la Bandari

0
40

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amekanusha habari zilizochapishwa na magazeti ya Nipashe na The Guardian vikieleza kuwa bunge limeridhia mkataba wa ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai.

Dkt. Tulia amesema azimio hilo kwa sasa bado lipo kwenye ngazi ya kamati ya pamoja kwa mujibu wa kanuni na mara baada ya kamati kumaliza kazi yake, azimio hilo limepanga kuingia bungeni Juni 10, 2023 kwa ajili ya mjadala na kupitishwa na bunge.

“Kwa mara nyingine tena tunatoa wito kwa waandishi wa habari na wanamitandao kuzingatia maadili kwa kuhakikisha kwamba wanajiridhisha na kupata taarifa sahihi kutoka kwa mamlaka zinazohusika kabla ya kutoa taarifa ili kuepusha taaruki na usumbufu kwa umma,” amesema.

TPA yakanusha kuipa DP World uendeshaii wa Bandari ya Dar kwa miaka 100

Aidha, amesema wakati wowote bunge lipo tayari kupokea, kujadili na kutoa maoni yao kupitia wananchi, yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa mipango ya Serikali.

Spika ameongeza kuwa, bunge litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita inayongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi na maendeleo ya Watanzania.

Send this to a friend