Dkt. Tulia: Chama cha Mapinduzi hakitaachia dola

0
41

Spika wa Bunge ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Tulia Ackson amesema hakuna siku itatokea chama hicho kitaachia nafasi ya kuitawala nchi kwa kuwa kimejiwekea mizizi imara katika kuwatumikia wananchi wake.

Ameyasema hayo Februari 04, 2023 akiwa kwenye ziara ya kichama Visiwani Zanzibar ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya CCM yaliyofanyika katika Mkoa wa Kusini Unguja.

Dkt. Tulia amesema ni wakati sahihi kwa wanachama wa chama hicho hususani vijana kuendelea kukipigania na kuwapigania viongozi wao wakuu akiwemo Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuyasemea mazuri anayoyafanya kwa nchi.

“Mwana CCM hupaswi kukaa kinyonge hata siku moja, kote Tanzania Bara na visiwani kuna miradi ya ujenzi wa shule kila kona, miundombinu ya barabara, zahanati, vituo vya afya n.k, haya yote ni mafanikio ya kujivunia, sasa unakaaje kinyonge? Tunaposema kwamba chama hiki hakitaachia dola tunamaanisha,” amesisitiza Dkt. Tulia.

Send this to a friend