Dkt Tulia: Wezi wa fedha za Serikali wamebuni mbinu mpya kuiba

0
37

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema ni dhahiri kuwa wezi wa fedha za serikali wamejifunza namna nyingine ya kutoa taarifa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kupatikana kwa hati safi kwenye maeneo yao.

Hayo yamedhihirika baada ya baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Bunda, Boniphace Getere kudhihirisha namna taarifa ya CAG iliyoitaja halmashauri hiyo kuwa na ubadhirifu mwingi licha ya kuwa miongoni mwa halmashauri zenye hati safi.

“Kwa namna ambavyo wabunge wameeleza halmashauri zao zilizo na changamoto, hizi hati 170 ni hati safi, na huu unaoitwa wizi, ubadhirifu umetokea kwenye hizo halmashauri.

Hizi hati safi zimetolewa kwa muktadha upi? Ni kwa maana ya kwamba zinakaguliwa kwa utaratibu ule wa kawaida na wamefuata taratibu za upelekaji wa taarifa kwa CAG, na kwa takwimu hizi zilizopo kwenye taarifa ya kamati na taarifa CAG, ni dhahiri hawa wabadhirifu wamejifunza namna nzuri ya kutoa taarifa,” amesema Dkt. Tulia.

Akiweka msisitizo Mbunge wa Viti Maalum, Anatropia Theonest wakati akiwasilisha taarifa kwa Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye ameeleza kuwa takwimu zinaonyesha baadhi ya mambo yamebadilika ikiwemo hata safi ukilinganisha na ripoti zilizopita, mbunge huyo amebainisha kuwa hati zimebadilika kutokana na wezi kujua namna nzuri ya kutumia risiti kuwasilisha vielelezo.

Send this to a friend