DP World yaongezewa mkataba upanuzi Bandari ya Maputo

0
37

Msumbiji imeidhinisha mkataba mpya kwa kampuni ya DP World Ltd. na Grindrod Ltd. kuendesha bandari yake kubwa huko Maputo hadi mwaka 2058, ambapo mkataba huo unajumuisha upanuzi wa bandari kwa gharama ya dola bilioni 2 [TZS trilioni 5], utakaosaidia kuvutia mizigo zaidi kutoka Afrika Kusini.

Kundi hilo, pamoja na shirika la reli la serikali ya Msumbiji, wamepewa miaka 25 zaidi ya kuendesha bandari hiyo ambapo uwekezaji wa karibu dola bilioni 1.1 unatarajiwa hadi mwaka 2033.

Upanuzi huo utaongeza uwezo wa bandari hadi tani milioni 54 kwa mwaka ifikapo 2058, ikilinganishwa na tani milioni 37 mwaka huu. Hii ni pamoja na kuongeza uwezo wa kusafirisha makaa ya mawe na kuongeza mara nne uwezo wa kushughulikia kontena za meli.

Bandari ya Maputo imekuwa ikikua kwa kasi, ikitumika kutoa huduma kwa uchumi unaoongezeka wa Msumbiji na kusaidia wachimbaji wa nchi jirani ya Afrika Kusini.

Send this to a friend