DPP afuta kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge Gekul

0
40

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Babati, Victor Kimario ameifuta kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea nayo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na kijana aliyedai kufanyiwa vitendo vya ukatili Hashimu Ally kupitia kwa wakili Peter Madeleka.

Kimaro amesema kuwa hakuna wakili wa Serikali aliyefika mahakamani wakati kesi hiyo ilipotajwa na taarifa hiyo iliwasilishwa Masijala.

Send this to a friend