
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na waasi wa M23 wameahidi kutafuta amani kufuatia majadiliano ya zaidi ya wiki moja nchini Qatar.
Mazungumzo hayo yaliyoratibiwa na Qatar yamekuja baada ya nchi hiyo kufanikisha mkutano kati ya Rais wa Congo, Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye anadaiwa kufadhili kundi hilo.
Viongozi wote wawili walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano baada ya mkutano huo.
Taarifa iliyotolewa baada ya mazungumzo nchini Qatar kati ya DRC na M23 imesema “Pande zote mbili zinathibitisha dhamira yao ya kusitisha uhasama mara moja, kukataa matamshi yoyote ya chuki, vitisho, na kutoa wito kwa jamii kutekeleza ahadi hizi.”