
Chadian soldiers gather on February 1, 2015 near the Nigerian town of Gamboru, just accros the border from Cameroon. In a deserted Gamboru, Chadian forces carried out clean-up operations after entering the town and retaking it from Boko Haram, which seized control months ago. AFP PHOTO / MARLE (Photo by MARLE / AFP)
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeomba msaada wa kijeshi kutoka Chad ili kupambana na waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.
Kwa mujibu wa afisa wa Chad na chanzo ndani ya Ikulu ya Congo, Waziri wa Uhusiano wa Kanda wa DRC alikutana na Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, na kufikisha ombi hilo kwa niaba ya Rais Felix Tshisekedi.
Chad imethbitisha mkutano huo kupitia Facebook, lakini haikutoa maelezo zaidi kuhusu mazungumzo yao. Afisa mmoja wa Chad amesema nchi hiyo inafikiria ombi la DRC, lakini bado haijafanya uamuzi wa mwisho.
Tangu Januari, waasi wa M23 wamechukua maeneo makubwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, wakidhibiti miji mikuu ya Goma na Bukavu. Serikali ya DRC inaituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao, madai ambayo Kigali inakanusha.