Droo ya 888 Bet kuwanufaisha vijana

0
46

Na, Mwandishi Wetu.

Kampuni mpya na nguli ya michezo ya kubahatisha iliyozinduliwa rasmi hivi karibuni ya 888 bet yawaasa wateja wake kuendelea kushiriki katika shindano la Dabodabo ili wajiweke karibu katika kinyanganyiro cha kuwania kitita cha milioni 100 taslimu za Kitanzania.

Hayo yamewekwa wazi na Balozi wa Kampuni hiyo James Tupa Tupa wakati alipokuwa akitangaza washindi watano waliopatikana kupitia droo ya shindano ya Dabodabo iliyofanyika jana na kuzawadia pikipiki, runinga pamoja na simu janja
“Mimi niendelee kuwasisitizia tu wadau wa michezo ya kubahatisha kuwa wasipotezee hii bahati ya kushiriki katika shindano letu la Dabodabo ya kila wiki kwani zawadi nyingi ikiwemo kitita cha Milioni 100 za Kitanzania, ambacho ataondoka nacho mshindi mmoja”, Alisema TupaTupa

Aidha, TupaTupa alisema kuwa kampuni ya 888 bet imekuja kuwaletea neema wadau wote ambao wanapendelea michezo ya kubashiri huku akisisitizia kuwa huu ndio mwaka wa kulala masikini na kuamka tajiri kwa kubashiri na 888bet.

Kwa upande mwingine, Kampuni ya 888bet ambayo imeingia rasmi Tanzania imekuwa miongoni mwa makampuni yenye lengo la kubadilisha michezo ya kubashiri kuwa fursa rasmi ya kutimiza ndoto za vijana kwa kuwapatia fursa ya kumiliki bodaboda kupitia ubashiri pekee.

Send this to a friend