Dulla Makabila aitwa BASATA kuhusu wimbo wake wa ‘Pita Huku’

0
78

Msanii wa Singeli, Dulla Makabila ameitwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa lengo la kwenda kujadili kuhusu wimbo wake mpya uitwao ‘Pita Huku’ ambao kwa sasa unashika namba moja ‘trending’ ukiwa na watazamaji wengi Youtube.

Msanii huyo amepata barua ya wito kutoka kwa Katibu Mtendaji, Dkt. Kedmon Mapana ambayo imesomeka kwamba “BASATA Inapenda kuwajulisha kwamba kutakuwa na kikao kitakachofanyika tarehe 21/12/2022 siku ya Jumatano, ajenda ya kikao ni kujadili kuhusiana na wimbo wako wa Pita Huku.”

Tanzania yavuna bilioni 12 kutokana na Kombe la Dunia

Aidha, baada ya wito huo Makabila ameandika katika ukurusa wake wa Instagram kwamba “nimepokea barua ya wito kutoka BASATA ambayo inahusu wimbo wangu mpya, wito nimeupokea na nitafika leo BASATA, nyie ni walezi wangu katika shughuli zangu za Sanaa. naimani utakua wito wa kheri.”

“Mashabiki zangu asanteni Kwa kuufanya wimbo wetu wa ‘Pita Huku’ kuwa trending number moja huko mjini Youtube, tuendelee kufuatilia kazi nzuri.”