Edward Lowassa alazwa Muhimbili

0
44

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo anaendelea na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji.

Mtoto wa mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa amesema baba yake amelazwa katika hospitali hiyo kwa takribani wiki moja sasa akiendelea kupatiwa matibabu.

“Baba alilazwa Muhimbili kama siku tano zilizopita. Alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya alipatwa na changamoto kidogo,” amesema mtoto huyo.

Fredrick amewaomba watanzania kuendelea kumuombea ili afya yake iendelee kuimarika.

Lowassa alihudumu kama Waziri Mkuu kuanzia mwaka 2005 hadi 2008 alipojiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi.

Send this to a friend