Elon Musk asema atajiuzulu akipata mtu mjinga wa kuchukua nafasi yake

0
42

Mmiliki wa kampuni ya Twitter, Elon Musk amesema atajiuzulu kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo pale atakapompata mtu mjinga vya kutosha kuchukua kazi hiyo.

Bilionea huyo aliahidi mapema kutii matokeo ya kura ya maoni ya Twitter ambayo asilimia 57.5 ya kura milioni 17, walipiga kura ya ndio kukubali ang’atuke katika nafasi hiyo.

“Nitajiuzulu kama Mkurugenzi Mtendaji mara tu nitapata mtu mjinga wa kuchukua kazi,” ameandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Aidha, mashirika ya kupigania uhuru wa kiraia pia yamekosoa mbinu yake ya kudhibiti maudhui, yakimtuhumu kuchukua hatua ambazo zitaongeza matamshi ya chuki na habari potofu.

Treni ya umeme kuendeshwa kwa umeme wa TANESCO

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya ulilaani kutokana na uamuzi wa kuwasimamisha kazi baadhi ya wanahabari wanaoripoti katika kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii.

Tangu Musk aliponunua mtandao wa Twitter mwezi Oktoba, amewafuta kazi takriban nusu ya wafanyakazi wake na kutangaza kuongeza kipengele cha kulipia cha uthibitishaji (verified) kwa watumiaji wa mtandao huo.

Send this to a friend