Elon Musk asubiri kibali cha TCRA kuwekeza nchini

0
19

Tovuti ya Starlink inayomilikiwa na mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa mtandao wa Twitter, Elon Musk imetangaza mpango wa kuleta huduma ya intaneti kwa njia ya satelaiti (starlink) nchi Tanzania kati ya Januari na Machi 2023 endapo itaruhusiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari amethibitisha kuwa kampuni hiyo ya Starlink ilituma maombi ya kutoa huduma ya intaneti nchini kupitia tovuti ya TCRA.

Chama cha Marubani chasema marubani hujiongoza wenyewe kutua Bukoba

Wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu huduma hiyo akiwemo mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abel Kinyondo ambapo amesema ikiwa huduma hiyo itafika nchini itasaidia wakulima kupata habari kuhusu hali ya hewa na jinsi wanavyoweza kuboresha mazao yao, pia itawasaidia wafanyabiashara kufanya biashara zao mtandaoni na kupata mafunzo yanayokusudiwa.

Teknolojia hiyo ya intaneti inapatikana baada ya kuunganishwa kwa satelaiti nyingi ambazo hutumika kutoa huduma ya intaneti kwenye maeneo mbalimbali duniani hasa vijijini.

Send this to a friend