Elon Musk awaambia Twitter wafanye kazi kwa saa nyingi au waache kazi

0
37

Mfanyabiashara na mmiliki wa mtandao wa Twitter, Elon Musk amewaambia wafanyakazi wa Twitter kuchagua kufanya kazi kwa saa nyingi na kwa hali ya juu au vinginevyo waache kazi.

Katika barua pepe iliyotumwa kwa wafanyakazi, imeeleza kuwa wanapaswa kukubaliana na masharti hayo ikiwa wanataka kusalia kwenye kampuni huku akiwataka wanaokubaliana nayo kujaza fomu maalum hadi kufikia Alhamisi Novemba 17, 2022 jioni.

Asilimia 65 ya wanawake Rwanda wanaamini ni sawa kupigwa na waume zao

Musk amebainisha kuwa wale wote ambao hawatajiandikisha kufikia Alhamisi, watapewa malipo ya miezi mitatu ya kuachishwa kazi na kuweka wazi kuwa Kampuni hiyo inahitaji kuwa imara zaidi ili kufanikiwa.

Mfanyabiashara huyo tayari amepunguza nusu ya wafanyakazi baada ya kuinunua Twitter na kutangaza saa 40 ya kazi kwa wiki huku akipiga marufuku kwa wafanyakazi kufanya kazi zao wakiwa majumbani.

Send this to a friend