Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi amekamatwa na polisi baada ya kujaribu kuvamia Bunge nchini humo kupinga kupanda wa gharama za maisha.
Omondi alikuwa pamoja na wanaharakati wengine waliofunga Barabara ya Bunge, katika Wilaya ya Kati ya Biashara (CBD) ya Nairobi huku wakiitaka serikali ya Kenya kupunguza bei ya bidhaa.
“Bado mapambano, mapambano, mapambano bado mapambano (mapambano yanaendelea),” kikundi hicho kikiongozwa na mwigizaji huyo kiliimba huku kikiwataka viongozi wa Chama cha Kenya Kwanza kuchukua hatua juu ya kupanda kwa gharama ya maisha.
Aina 6 za Smartphones bora zaidi unazoweza kununua
Katika maandamano hayo kundi hilo liliungwa mkono kutoka kwa viongozi wa Azimio la Umoja ambalo liliwataka Wakenya kuungana nao kuisisitizia Serikali ya Rais William Ruto juu kupunguza kwa gharama hizo.
Hata hivyo, juhudi zao za kuvamia majengo ya Bunge zilizimwa baada ya maafisa waliokuwa wakilinda eneo hilo kutuliza kundi hilo la waandamanaji.
Mfumuko wa bei umeathiri kwa kiasi kikubwa bei ya bidhaa. Rais William Ruto awali aliahidi kupunguza gharama ya maisha hasa bei ya bidhaa muhimu kama unga, mafuta ya kupikia, mkate na sukari.
Bei za sasa za rejareja za unga ni Ksh195 [TZS 3,700], huku Kilo moja ya sukari ikiuzwa Ksh146 [TZS 2,700], lita 1 ya mafuta ya kupikia ni Ksh360 [TZS 6,700].