Ester Matiko ataka wanaobaka na kulawiti wahasiwe

0
61

Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Ester Matiko ameishauri serikali kutafuta njia nzuri ya kukomesha vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto ikiwemo kuondoa viungo vinavyofanya vitendo hivyo na wote wanaohusika wahasiwe.

Akichangia mjadala huo bungeni Dodoma, mbunge huyo amesema kuna haja ya Serikali kufanya maboresho ya sheria ili kuwe na adhabu kali zaidi dhidi ya wote wanaonajisi watoto ili kuwa fundisho kwa wengine.

“Vitendo vya kulawiti na kubaka vimekithiri nchini, ingetakiwa wanaofanya vitendo hivyo kuhasiwa au kuondoa viungo vinavyofanya vitendo hivyo,” amesema Matiko.

Hata hivyo wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni aliliambia Bunge kuwa jumla ya matukio 27,838 ya vitendo vya ukatili nchini yameripotiwa kwenye vituo vya polisi katika miaka minne iliyopita, huku matukio ya ubakaji yakiongoza kwa idadi ya 19,726.

Send this to a friend