EWURA: Agizo la Rais Samia lashusha bei ya mafuta

0
49

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli yaliyopita Bandari ya Dar es Salaaam ambapo yamepanda kwa TZS 12/lita, badala ya TZS 145/lita ambayo ilitakiwa kutozwa kuanzia Oktoba 6, 2021.

Punguzo hilo la TZS 133 limetokana na serikali kupunguza tozo nane kwenye mafuta.

Kaimu Mkurugenzi wa EWURA, Godfrey Chibulunje amesema hayo leo jijini Dodoma na kueleza kwamba kama kusingekuw ana punguzo kama ambavyo Rais Samia Suluhu ameeleza, basi bei ya petroli ingepanda kwa shilingi 145.

Kutokana na punguzo hilo, bei ya mafuta ya petroli kwa mkoa wa Dar es Salaam itauzwa TZS 2,439/lia, dizeli TZS 2,261/lita na mafuta ya taa TZS 2,188/lita. Ameeleza kwa Arusha bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakuwa ni TZS 2,535. lita, 2,302/lita na 2.272/ lita mtawalia.

Kwa mkoa wa Pwani Petroli, dizeli na mafuta ya taa zitauzwa TZS 2,443/lita, TZS 2,226/lita na TZS 2,192/lita, mtawalia, wakati Dodoma bei itakuwa petroli ni 2.497/lita, dizeli 2.320/lita na mafuta ya taa 2,246/lita.

Send this to a friend