EWURA: Hakuna uhaba wa mafuta nchini

0
15

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeihakikishia Serikali na Watanzania kwa ujumla kuwepo kwa mafuta ya kutosha nchini na kwamba kila eneo litafikiwa na wataendelea kupatiwa huduma ya mafuta kama kawaida.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, January Makamba alipotembelea kuona zoezi zima la upokeaji na usambazaji wa mafuta nchini, amewataka wenye vituo vya mafuta vya kuuza rejareja nchini wahakikishe wanakuwa na mikataba na wauzaji wa mafuta ya jumla ili kuwa na uhakika wa kupata bidhaa hiyo wakati wote.

“Tumekubaliana kwamba ifikapo tarehe 31 kila mwenye kituo na kwa mujibu wa masharti ya leseni aliyopewa ni kwamba atahakikisha kwamba walau ameingia mkataba na wauzaji wa mafuta wa jumla wawiili na mikataba hiyo itawasilishwa EWURA,” amesema.

Akijibu swali la Waziri wa Nishati, January Makamba kuhusu tetesi za ukosefu wa mafuta nchini, Mkurugenzi Mkuu Mount Meru, Charles Maingu amewahakikishia uwepo wa mafuta na kueleza kuwa endapo kuna sehemu za pembezoni ambapo watu wanafikiria hakuna mafuta basi wapewe taarifa ili waweze kuwahudumia.

Kwa upande wa wasambazaji wa mafuta wameihakikishia Serikali kuwepo kwa mafuta ya kutosha na hakuna uhaba wa mafuta nchini tofauti na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

“Napenda niwahakikishie mafuta yapo ya kutosha. Tuna dizeli zaidi ya lita milioni 12 kwenye matenki tuna petrolli zaidi milioni 5 kwenye matenki lakini bado tunaendelea kupokea, tuna mzigo wa lita milioni 80 ambao tunategemea kuupokea kuanzia wiki ijayo mpaka Agosti 23,” amesema Fatma Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji Puma Energy Tanzania.

Send this to a friend