EWURA yavifungia vituo vingine vitatu vya mafuta

0
44

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imevifungia vituo vitatu vya mafuta kwa muda wa miezi sita baada ya kubainika kutouza mafuta kwa maslahi binafsi.

Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, Dkt. James Andilile amevitaja vituo hivyo kuwa ni Camel Oil kilichopo Gairo mkoani Morogoro, Petcom killichopo Mbalizi mkoani Mbeya na Rashal Petroleum Ltd kilichopo Mkalama mkoani Singida baada ya EWURA kuvifanyia uchunguzi na hivyo kukamlisha idadi ya vituo vitano vilivyofungiwa.

“Kutokana na ufichaji wa mafuta, EWURA inavichukulia hatua vituo nane ambavyo vimejihusisha na tabia ya kuficha mafuta. Hivyo basi Septemba 4, 2023 EWURA ilivifungia vituo viwili vya Camel Oil Msamvu, Morogoro na Matemba cha Turiani kwa miezi sita,” amesema.

Nchi 10 za Afrika zenye bei ya juu zaidi ya mafuta kwa mwezi Septemba

Aidha, EWURA imesema ilikuwa inavichunguza vituo vingine sita vilivyoonesha kutofanya biashara ya mafuta kwa sababu mbalimbali ambapo uchunguzi umebaini kuwa vituo vitatu kati ya hivyo vimebainika kwenda kinyume na taratibu za EWURA.

Send this to a friend