EWURA yavifungia vituo viwili kwa kuficha mafuta

0
58

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kuvifungia vituo vingine viwili kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kuhodhi mafuta kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu.

Vituo vilivyofungiwa ni kituo cha Kipenda Roho Investment kilichopo Soya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma pamoja na kituo cha Oilcom kilichopo Soya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.

Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo amesema uamuzi huo umefanywa baada baada ya kupitia utetezi wao katika kikao kilichofanyika Oktoba 09, mwaka huu na kujiridhisha kuhusika na kitendo hicho.

“Kwa uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi, hadi sasa utakuwa umegusa vituo tisa (9) na bado uchunguzi unaendelea kwa vituo vingine,” amesema.

Aidha, EWURA imetoa onyo kwa OMCs na wamiliki wa vituo vya mafuta kuwa serikali iko macho na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayevunja sheria.

Send this to a friend