Ex wa Bibi Harusi amtumia zawadi ya bomu kwenye harusi, wawili wajeruhiwa

0
65

Wanandoa wawili katika kijiji cha Mindhabari, nchini India wamejikuta kwenye matatizo baada ya aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Bibi Harusi, Raju Patel kutuma zawadi ya bomu kwenye harusi yao.

Bomu hilo lililofichwa kwenye mdoli lililipuka wakati wanandoa hao wakifungua zawadi siku ya pili baada ya harusi yao, ambapo mume wa bibi harusi pamoja na mpwa wake (3) walijeruhiwa vibaya.

“Lililipuka mara tu zawadi ilipofunguliwa na macho ya mkwe wangu yote mawili kuharibika, nifanye nini sasa? Naweza kutoa jicho moja kwa mkwe wangu,” alisema Baba mkwe.

Binti amshtaki ‘baba mkwe’ kwa kukataa asiolewe na kijana wake

Baada ya mahojiano na polisi mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo na kudai alitaka kuwafundisha somo kwa kuwapa zawadi ya namna hiyo.

Send this to a friend