Facebook kutumia TZS trilioni 2 kuwalipa watakaotumia Reels

0
43

Facebook inakusudia kuweka mfumo wake wa video fupi (Reels) kwenye ukurasa wa nyumbani (News Feed) wa watumiaji wake ili kuongeza kuonekana na matumizi yake ikiwa ni mkakati wa kupambana na kasi ya ukuaji wa mtandao wa TikTok.

Ili kuwa vutia watu wenye ushawishi (influencers) kutumia Reels, kampuni hiyo inakusudia kutoa malipo yenye jumla ya TZS trilioni 2.3 kwa mwaka wote wa 2022 kwa baadhi wa watengeneza maudhui watakaochapisha video zao Facebook au Instagram, ambapo Reel ilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2020. Kwa sasa Facebook inatoa malipo hayo kwa watu wachache (invite-only group). Hata hivyo mtandao huo haujaeleza utatumia utaratibu gani kwenye malipo hayo.

Tiktok ambayo inatishia ukubwa wa Facebook imejikusanyia mamilioni ya watumiaji, wengi wao wakiwa ni vijana. Kuimarika huko kwa TikTok kunatafsiri kuwa ni tishio kwa Facebook ambao ndio mtandao wa kijamii wenye watumiaji wengi zaidi. Aidha, kukua huko kwa TikTok kumetajwa pia kuwa sababu ya Mtandao wa Instagram kufanya vibaya.

Facebook inapambana kuidhibiti TikTok ambapo inadaiwa wanataka kuigeuza Instagram kuwa mtandao wa unaojikita zaidi kwenye maudhui ya video.

Kuweka Reels kwenye News Feed kunalenga kuongeza idadi ya watu inaowafikia kwa kuonekana kwa watu ambao pia huenda hawajui au hawapendelei huduma hiyo.

Takribani watu bilioni 2 duniani kote hutumia Facebook kila siku, hata hivyo umri wa watumiaji hao umesonga. Utafiti wa hivi karibuni (Pew Research) umebainisha kuwa 77% ya watu wazima kati ya maika 30 na 49 wanatumia Facebook na 73% ya watu wazima kati ya 50 na 64 wanatumia mtandao huo, lakini ni chini ya robo ya watu kwenye makundi hayo wanaotumia TikTok.

Pia, Facebook inaangalia ni kwa namna gani inaweza kutengeneza fedha kwa kuweka matangazo kupitia video za Reels.

Send this to a friend