Facebook yadaiwa kuwafuatilia watumia wa Instagram kupitia kamera za simu

0
35

Kampuni ya Facebook imeshitakiwa kwa tuhuma za kuwafuatilia watuamiaji wa Instagram kwa kutumia kamera za simu zao bila ridhaa ya watumiaji.

Kesi hiyo imetokana na ripoti za vyombo vya habari kuwa mtandao huo wa kushirikishana picha umekuwa ukitumia kamera za simu za iPhone hata pale ambapo watumiaji wa simu hizo hawatumii kamera.

Facebook imekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa kulikuwa na hitilafu ya programu (bug) ambayo inairekebisha. Imesema kuwa ‘bug’ hiyo ilikuwa ikitoa taarifa (notification) kwa watumiaji wa Instagram kuwa iPhone inatumia kamera zao, jambo ambalo halikuwa kweli.

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa New Jersey, Marekani, mtumiaji wa Instagram ambaye ni mlalamikaji, Brittany Conditi amesema kuwa programu hiyo (Facebook) inatumia kamera za iPhone kwa makusudi ili kukusanya taarifa za siri watumiaji ambazo hawawezi kuzikusanya kwa njia nyingine.

Katika kesi nyingine iliyofunguliwa mwezi uliopita Facebook ilituhumiwa kutumia teknolojia ya utambuzi wa sura (facial-recognition) kukusanya taarifa (biometric data) za watumiaji wa Instagram zaidi ya milioni 100 kinyume na sheria. Hata hivyo kampuni hiyo ilikanusha madai hayo kwa maelezo kuwa Instagram haitumii teknolojia hiyo.

Send this to a friend