Fahamu Aina za makundi ya damu, nani unayeweza kumchangia au kukuchangia damu

0
90

Wataalamu wa afya wanashauri ni muhimu binadamu kujua kundi lake la damu ili iweze kumsaidia wakati atakapohitaji kupata matibabu ambayo yanahitaji damu au kumsaidia mtu anayehitaji damu.

Damu ya binadamu imegawanyika katika makundi makuu manne, ambayo ni A, B, AB, na O.

Ili kundi la damu liwe A ni lazima ukuta wa chembechembe nyekundu za damu ubebe taarifa za antijeni A, kundi B liwe na antijeni B, kundi AB liwe na antijeni zote mbili yaani A na B kwa pamoja, na kundi O huwa halina antijeni yoyote.

Aidha, Makundi ya damu ni lazima pia yawe chanya au hasi. Ukiachia taarifa za antijeni A au B ambazo huwepo kwenye ukuta wa chembechembe nyekundu za damu, sehemu hii hubeba pia aina moja ya protini inayoitwa Rh factor D, au maarufu zaidi kama RhD.

Ikitokea protini hii ipo kwenye chembechembe nyekundu za damu, kundi husika la damu litakuwa chanya, na ikitokea protini hiyo haipo basi kundi husika litakuwa hasi.

Ili uweze kupokea damu, ni lazima kundi lako husika lifanane na kundi la mtu anayechangia damu hiyo. Fuatilia orodha hii ili kufahamu;

KUNDI ANATOA ANAPOKEA
A+ A+, AB+ A+, A-, O+,O-
A- A+, A-, AB+, AB- A-, O-
B+ B+, AB+ B+, B-, O+, O-
B- B+, B-, AB+, AB- B-, O-
AB+ AB+ Kila kundi
AB- AB+, AB- AB-, A-, B-, O-
O+ A+, B+, AB+, O+ O+, O-
O- Kila kundi O-