Fahamu dalili na namna ya kujikinga na Homa ya Nyani (Monkeypox)

0
84

Wizara ya Afya imetoa tahadhari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nyani (Monkeypox) ambao umetamalaki nchi mbalimbali duniani.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema, ugonjwa wa Homa ya Nyani huambukizwa kutoka kwa mnyama mwenye maambuki kwenda kwa binadamu, na kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu endapo mtu asiye na maambukizi atagusana na mtu mwenye maambukizi.

“Mnamo tarehe 16 Mei 2022, Shirika la Afya Duniani lilitoa taarifa ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa ‘Monkeypox’ nchini Uingereza. Mpaka kufikia tarehe 20 Mei, 2022 watu 38 walikuwa wamekwisha thibitika kuwa na ugonjwa huo kutoka nchi mbalimbali duniani,” amesema.

Aidha, ametaja dalili kuu za ugonjwa huo ikiwa  ni pamoja na homa, vipele vinavyoweza kuwa na majimaji au usaha hasa sehemu za uso, viganja vya mikono na nyayo za miguu, mwili kuchoka na kichwa kuumwa.

Majaliwa amsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Arusha

Dalili za ugonjwa hudumu kati ya wiki mbili mpaka nne, na kwa kawaida ugonjwa huwa si mkali na wakati mwingine hufanana na Tetekuwanga na mtu hupona bila dawa yoyote.

Mara chache ugonjwa huo unaweza kuwa mkali zaidi na kupelekea kifo hasa kwa watoto wachanga na watu wenye magonjwa yanayodhoofisha kinga ya mwili.

Mollel amesema nchini Tanzania hakuna mgonjwa wa ‘Monkeypox’ aliyewahi kugundulika na kutoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yale ya mlipuko ikiwa ni pamoja na usafi binafsi na usafi wa mazingira.

Send this to a friend