Fahamu faida 5 za kunywa maji moto asubuhi

0
67

Baadhi ya watu husema unywaji wa maji ya moto umewasaidia kupunguza vitambi na unene, huku wengine wakitibu maumivu ya viungo na uchovu kwa kutumia maji hayo.

Watalam mbalimbali wa afya duniani wameeleza faida za unywaji wa maji ya moto asubuhi na jinsi yanavyoweza kukukinga na magonjwa.

Daktari George Munisi, Mtaalamu wa Chakula na Lishe anasema unywaji wa maji ya moto wakati wa asubuhi unasaidia sana kuamsha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

“Kuna vitu vinaitwa vichocheo vya mfumo wa chakula, unapokunywa maji ya moto wakati wa asubuhi unavisaidia kufanya kazi katika efficient (ufanisi),” anasema Dkt. Munisi.

Baadhi ya faida zilizotajwa ni pamoja na;

Kupunguza mafuta mwilini
Wataalamu wa masuala ya chakula na lishe wanasema kuna uhusiano kati ya unywaji wa maji ya moto na kupungua kwa mafuta mwilini.

“Unapotumia maji ya moto wakati wa asubuhi yanaenda kuyeyusha mafuta yaliyojikusanya kwenye utumbo kwa kiasi fulani,” ameeleza

Mbali na maoni ya mtalaam huyo, tovuti ya habari za afya zimetaja manufaa mengine ambayo mtu anaweza kuyapata endapo akinywa maji ya moto wakati wa asubuhi mbali na kupunguza uzito na unene.

Kupunguza hatari ya kupata choo kigumu (Constipation)
Upungufu wa maji mwilini husababisha chakula kujikusanya kwenye utumbo mpana kabla ya kutoka nje kama haja kubwa. Hivyo unywaji wa maji ya moto wakati wa asubuhi utakuweka kwenye nafasi nzuri ya kuepuka changamoto ya kupata choo kigumu.

Haya ndiyo madhara ya kuchelewa kula chakula usiku

Huimarisha mzunguko wa damu mwilini
Kuanza siku yako na maji ya moto hufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri ambao utakuweka kwenye nafasi nzuri ya kuepuka magonjwa ya moyo.

Kupunguza msongo wa mawazo
Kwa mujibu wa tovuti ya Medical News Today, kunywa vinywaji vya moto asubuhi kama chai, kahawa na maji ya moto kunaweza kupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi.

Maji ya moto huondoa sumu mwilini
Wataalamu wa afya wanasema maji ya moto huufanya mwili utokwe jasho hivyo kuna nafasi kubwa ya kupoteza sumu mwilini ambazo hutoka kwa njia ya jasho na mkojo.

JE! Huwa unakunywa maji ya moto asubuhi?

Send this to a friend